Jumamosi 19 Aprili 2025 - 17:54
Sifa za Imam; Mwenye elimu kubwa zaidi na uelewa mpana zaidi miongoni mwa watu

Hawzah/ Imam ambaye anachukua nafasi ya uongozi na uwatawala kwa watu, ni lazima aijue dini kwenye nyanja zake zote na awe na uelewa kamili wa sheria zake, vilevile aweze kujibu maswali yote ya watu katika maudhui tofauti, na awaongoze kwenye njia bora zaidi kadri iwezekanavyo.

Shirika la Habari la Hawza | Mrithi wa Mtume (rehema na amani zimshukie yeye na Ahli zake), ambaye ni dhamana ya kuendelea uhai wa dini na mwenye jukumu la kujibu mahitaji ya mwanadamu, ni mtu mwenye haiba ya kipekee ambaye kutokana na nafasi yake kubwa katika uongozi na na cheo chake kidini anakuwa na sifa mahsusi, muhimu zaidi katika sifa hizo ni:

Taqwa (uchaji-Mungu); uwezo wa kuongoza mjumuiko wa wanadamu na kuendesha mambo ipasavyo kwa mujibu wa mafundisho ya dini; kuwa na sifa ya isma (kutokukosea kabisa) kiasi kwamba hata kosa dogo hawezi kulitenda; na vilevile elimu na maarifa yanayotokana na elimu ya Mtume (rehema na amani zimshukie yeye na Aali zake) elimu ambayo imeunganishwa na elimu ya Mwenyezi Mungu.
Kwa hivyo Imam huwa ni mwenye uwezo wa kujibu kila jambo katika nyanja zote.

Kwa kuzingatia sifa hizi zilizotajwa kwa ajili ya Imam, ni jambo lililo wazi kuwa kumchagua mtu wa namna hii hakuwezi kufikiwa kwa uwezo na maarifa ya wanadamu, bali ni Mwenyezi Mungu tu ambae kwa elimu yake isiyo na mipaka anaweza kuwachagua viongozi na warithi wa Mtume. Hivyo basi, miongoni mwa sifa muhimu zaidi za Imam ni kuwa ameteuliwa na Mwenyezi Mungu.

Kwa kuzingatia umuhimu wa sifa hizi, tutazieleza kwa muhtasari moja baada ya nyingine:

Elimu ya Imam:
Imam ambaye anashika nafasi ya uongozi na kuwaongoza watu, ni lazima aijue dini kwa ukamilifu, na awe na uelewa kamili wa sheria zake. Vilevile, kwa kuijua tafsiri ya aya za Qur’ani na kuwa na uelewa wa kina kuhusu Sunna ya Mtume (s.a.w), anaweza kufafanua maarifa ya dini na kujibu maswali yote ya watu katika maudhui na nyanja mbalimbali, na kuwaongoza kwenye njia iliyo bora zaidi.

Ni jambo lililo dhahiri kuwa, rejea ya kielimu ya aina hiyo inaweza kuwa tegemeo na nguzo kwa watu, na uungwaji mkono wa kielimu wa namna hiyo unaweza tu kuwepo kwa njia ya kuunganishwa na elimu ya Mwenyezi Mungu. Ndiyo maana Shia wanaitakidi kuwa elimu ya Maimam na warithi halisi wa Mtume (s.a.w) imetokana na elimu isiyo na mipaka ya Mwenyezi Mungu.

Imam Ali (a.s) anasema kuhusiana na alama alizonazo Imam wa haki:

“Imam ni mtu mwenye elimu kubwa zaidi kuhusu halali na haramu ya Mwenyezi Mungu, hukumu mbalimbali, amri na makatazo yake, na kila kitu ambacho watu wanakihitaji.”
(Mizan al-Hikmah, juzuu ya 1, hadithi ya 861)

Utafiti huu unaendelea…

Imenukuliwa kutoka katika kitabu (Negin-e Aferinesh), pamoja na kufanyiwa mabadiliko kiasi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha